Back to top

Spika Ndugai amesitisha uwakilishi wa Masele Bunge la Afrika

16 May 2019
Share

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemwita nyumbani Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mhe.Stevene Masele kutokana kutumia nafasi hiyo vibaya na hivyo kuharibu taswira nzuri ya nchi.

Taarifa hiyo ya kuitwa nyumbani kwa Mhe.Masele ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi imetolewa na Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai bungeni kabla ya kuanza kwa shughuli za bunge tofauti na dua.

Mhe.Ndugai amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemwandikia barua Rais wa Bunge la Afrika Mashariki kuhusu kusitisha ushiriki wa Mhe.Masele katikia bunge hilo hadi atakaporudi nyumbani kuja kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki na Madaraka ya Bunge pamoja na Kamati ya Maadili ya Chama chake.

Mhe.Ndugai amesema Mhe.Masele licha ya kuitwa nyumbani kuja kuhojiwa na kamati hiyo amekuwa akikaidi na ndio maana bunge limefikia hatua ya kuandika barua kuomba ushiriki wake usitishwe kwa muda.

Amesema mbali na mambo mbalimbali ambayo Mhe.Masele amekuwa akifanya moja ya jambo ambalo amekuwa akifanya lisilokuwa la kiuungwana ni kuigonganisha mihimili ya dola na ushaidi wa mambo hayo yapo.