Back to top

SUMATRA,Jeshi la polisi na TABOA wasema hakuna mgomo wa madereva

14 May 2019
Share

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nje kavu-SUMATRA na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani imetangaza hakuna mgomo wa madereva wa mabasi ya mikoani uliotarajiwa kufanyika kesho mei 15 na kuwataka madereva kote nchi kufanyakazi yao kwa mujibu wa sheria na kanuni za usafiri wa barabarani.

Kwa upande wao wakizungumzia mgomo huo, mwakilishi wa chama cha madereva wa mabasi TABOA Bwana Issa Nkya ameitaka SUMATRA na kikosi cha usalama barabara kutatua changamoto zinazojitokeza haraka iwezekanavyo hasa katika mkoa wa Morogoro.

Awali chama cha madereva wa mabasi kilijipanga kuitisha mgomo wa madereva kuanzi kesho kushinikiza serikali kutatua changamoto ya adhabu zinazotozwa na SUMATRA kufuatia mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi barabarani kutokana na kuwatoza faini kubwa madereva na kulazimika kuyatelekeza mabasi na usumbufu kwa abiria.