Back to top

Taasisi na wananchi watakiwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa.

23 March 2019
Share

Taasisi za serikali na zisizo za serikali pamoja na watu binafsi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini katika kupanga na kufanya maamuzi kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii sambamba na kuchukuwa tahadhari zinazoweza kuepusha majanga yasio ya lazima.

Hayo yamebainishwa na waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe katika kilele cha maadhimisho ya siku ya hali ya hewa duniani yenye kauli mbiu isemayo jua dunia, hali ya hewa ambapo Mhandisi Kamwele amesema taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa endapo zitatumiwa vyema zinaweza kuepusha hasara na madhara mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika maeneo ambayo huitaji taarifa hizo kwa maendeleo ya kiuchumi na jamii.

Mamlaka ya viwanja vya ndege(TAA),mamlaka ya usafiri wa anga pamoja (TCAA)na shirika la wakala wa meli Tanzania(TASAC) ni miongoni mwa taaasisi zinazotegemea sana taarifa za hali ya hewa katika utendaji wake ambapo baadhi ya viongozi wa taasisi hizo wamesema taarifa hizo ni muhimu kwa kua utoaji wa huduma zao kwa wananchi hutegemea sana taarifa za hali ya hewa.