Back to top

Tabora, Kigoma na Rukwa inaongoza kwa uharibifu wa mazingira.

14 May 2019
Share

Mikoa ya Tabora, Kigoma na Rukwa inayounda kanda ya Magharibi imetajwa kuwa inaongoza kwa uharibifu wa mazingira nchini kwa asilimia thelathini na tano kutokana na shughuli za kilimo cha kuhama hama, ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa, pamoja na shughuli za ufugaji.

Mratibu wa Kituo cha Kimataifa cha Ufuatiliaji wa Hewa Ukaa Profesa Eliakimu Zahabu amesema hayo baada ya uzinduzi wa kikao cha kwanza cha bodi ya mpito ya Kituo cha Taifa cha Kuratibu Hewa Ukaa.