Back to top

Tangawizi kuuzwa kwa stakabadhi ghalani kumnufaisha mkulima.

21 November 2019
Share

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametangaza zao la tangawizi mkoani humo litauzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia ushirika, ili kumnufaisha mkulima.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakulima wa zao hilo wa kata ya Mkongonotema katika  Halmashauri ya wilaya Madaba inayolima tangawizi kwa wingi mkoani Ruvuma.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Pololet Mgema amesema ushirika ni njia sahihi ya kumkomboa mkulima na kuwataka viongozi wa ushirika Songea kuacha kuwaibia wakulima.

Hata hivyo, wakulima na wadau wa zao la Tangawizi wameelezea wasiwasi wao wa kufaidika na kilimo cha zao hilo linaloharibika haraka tofauti na mazao mengine.