Back to top

Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa 39 wa SADC Agosti.

13 June 2019
Share

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC utakaofanyika mwezi Agosti mwaka 2019 jijini Dar es salaam.
 
Mkutano huo utatanguliwa na vikao vya awali kwaajili ya maandalizi na kutangulia kwa wiki ya maonyesho ya bidhaa za ndani ujulikanao kama wiki ya viwanda ya SADC 22-26 Julai.

Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa nchi 16 zinazounda jumuiya ya SADC. 

Mara ya mwisho nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo ilikuwa mwaka 2003 ambapo Rais Benjamini Mkapa alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo. 

Yamesemwa na Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Profesa Palamagamba kabudi.