
Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa ameitaka jamii ya Tanzania kujifunza,kuielewa na kuitekeleza sheria ya watu wenye ulemavu kutokana na watanzania na baadhi ya viongozi kutokuijua vizuri ilihali kuna sera nzuri
Amesema hayo katika kikao cha mashauriano juu ya masuala ya watu wenye ulemavu iliyoshirikisha wizara, wadau na viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu na kusema mpaka sasa serikali imefanya ukarabati wa shule za serikali 45 ambao umezingatia miundombinu ya watu wenye ulemavu.
Nae mmoja wa mwakilishi wa chama cha viziwi Tanzania Bi. Lupy Mwaswanya ameomba kuwe na utambuzi wa awali wa watu wenye ulemavu ili kutoachwa nyuma katika elimu ya uzazi.
Aidha waziri Stella ameendelea kusisitiza kuzingatia sheria namba 9 ya watu wenye ulemavu hususani katika miundombinu bora ya majengo jumuishi.