Back to top

TCRA imetoa leseni 45 kwa watoa huduma wa maudhui.

25 May 2018
Share

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetoa leseni 45 kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mitandao huku ikiwataka kuzingatia maudhui sahihi katika kazi zao za utoaji wa taarifa.

Mkurugenzi mkuu wa TCRA Eng James Kilaba pamoja na masuala mengine amewataka watoa hudumahao waliopata leseni kuwa mabalozi wazuri huku akiwasisitiza kuhakikisha wanazingatia  matumizi sahihi ya maudhui na kwamba tayari TCRA imekwisha kutekeleza matakwa ya kanuni za maudhui mtandaoni ya mwaka 2018  hasa kanuni ya nne.

Miongoni mwa watoa huduma waliopata leseni  hizo ni pamoja NA ITV, RADIO ONE, CAPIATL TV, CAPITAL RADIO, na ITV POPOTE.

Tangu kutangazwa kwa utaratibu wa utoaji wa leseni maombi zaidi ya 262 yaliwasilishwa,ambapo maombi zaidi ya ya 170 hayakukidhi vigezo,ambapo ni maombi 45 pekee ndio yaliyopatiwa leseni.