Back to top

Tetemeko la ukubwa wa 5.2 vipimo vya richter latokea Katavi.

09 September 2019
Share

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 5.2 wa vipimo vya richter limetokea katika mkoa wa Katavi majira ya alfajiri.

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga amesema hakuna madhara yaliyoripotiwa kwa  binadamu au mali kuharibiwa.

Hata hivyo amekiri kuwepo kwa taharuki kidogo kwa baadhi ya wananchi na sasa wanaendelea na shughuli zao.

Kwa mujibu wa mjiolojia Mwandamizi Gabriel Mbogoni tetemeko hilo limedumu kwa dakika tatu na limepita karibu katika wilaya zote za mkoa wa Katavi.

Amesema tofauti na majanga mengine tetemeko halina dalili za mapema wala viashiria vya kuweza kutoa tahadhari eneo husika.