Back to top

TPA kujenga bandari kavu Inyala, Mbeya.

24 June 2019
Share

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) inampango wa kujenga bandari kavu katika eneo la Inyala, Mbeya ili kuhudumia wateja wa Zambia, Congo DRC na wafanyabiashara wa Tanzania kutoka nyanda za juu kusini.

Akijibu swali la mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza ambapo pamoja na mambo mengine ameuliza ni lini ujenzi wa bandari kavu ya Inyala utaanza na wananchi watalipwa fidia.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe.Atashasta Nditiye amesema ujenzi wa bandari kavu utasaidia kukabiliana na ushindani na bandari za nchi jirani.

Amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 TPA imepanga kufanya upembuzi yakinifu katika eneo lenye ukumbwa wa ekari 100 ili kubaini mahitaji halisi na eneo linalofaa ili bandari kavu inayojengwa iweze kuleta tija.

Aidha amesema mpango wa serikali kupitia TAZARA ni kufanya upembuzi yakinifu kwa lengo la kutandika reli kuelekea kwenye eneo litakalojengwa bandari kabu ya Inyala mpango ambao unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2020/21.