Back to top

Ugonjwa wa Dengue waendelea kuwa tishio kwa wakazi wa Dar

23 May 2019
Share

Wakati ugonjwa wa homa ya Dengue ukiendelea kuwa tishio kwa wakazi wa Dar es Salaam wananchi wameiomba serikali kuharakisha zoezi la kuingiza gharama za matibabu kwenye mfumo wa taifa ya bima ya afya.

Licha ya jitihada za kujikinga na ugonjwa huo zikiendelea kwa baadhi ya wakazi wa jiji hilo wamesema wana hofu ya matibabu kwa njia ya pesa taslimu.

Kijana Ismail Ramadhan ambaye ni mwendesha bajaj eneo la Upanga ameugua ugonjwa wa Dengue ambapo amesema kwa mara ya kwanza alihisi ana malaria hivyo kwa hali aliyokuwa akijihisi aliamua kuangalia dalili za ugonjwa huo kwenye mitandao ya kijamii ndipo alipokimbia hospitali haraka, amesema ilibidi atumie akiba yake kwa ajili ya matibabu.

Taarifa ya serikali nchini kupitia wizara ya afya inaeleza kuwa jumla ya wagonjwa 1,237 wamegundulika na ugonjwa huo huku jiji la Dar es Salaam likiongoza kwa kuwa na wagonjwa.