Back to top

Ukosefu wa maji katika mabwawa mapya wakamwisha kuhamishwa viboko

20 November 2019
Share

Changamoto ya upatikanaji wa maji katika mabwawa mapya yaliyochimbwa katika hifadhi ya taifa ya Katavi kwa ajili ya kuhamisha wanyama aina ya viboko walio katika bwawa la Milala katika manispaa ya Mpanda umesababisha kuchelewa kuanza kwa zoezi la kuwahamisha wanyama hao

Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya uhifadhi wa wanyama pori nchini (TAWA) Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko, amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya jeshi usu katika kituo cha mafunzo Mlele

Willium Mwakilema ni naibu kamishna wa uhifadhi na maendeleo ya biashara (TANAPA) amesema tayari wameshachimba mabwawa matatu pembezoni mwa mto Ikuu yaliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 341