Back to top

Urasimu na Rushwa vyamshtua CHALAMILA, ampa siku 5 M/Halmashauri Mbeya

20 November 2019
Share


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Albert Chalamila ametoa siku tano kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kutoa kibali cha kupata ardhi kwa muwekezaji anayetaka kujenga kiwanda cha mbegu mkoani humo anayedaiwa kutaka kuhamisha mradi huo kwenda mkoa mwingine kwa sababu ya urasimu ambao umemchelewesha kupata kibali hicho.

Akikagua ujenzi wa kiwanda cha kipya cha kusindika maziwa kinachojengwa wilayani Rungwe amesema urasimu na rushwa unakwamisha miradi mingi mkoani Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Bwana Julius Chalya amesema halmashauri ya wilaya hiyo inazalisha zaidi ya lita milioni sitini na mbili kwa mwaka lakini ni asilimia kumi na moja tu ya maziwa hayo yanauzwa katika mfumo rasmi na yaliyosalia yanauzwa kwa njia za panya.