Back to top

Vibali vya TMDA kulipiwa Kielekitroniki mpaka wa Namanga.

21 November 2019
Share

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) imeweka mfumo wa kielektroniki katika kituo cha forodha cha Namanga wa kuwawezesha wafanyabiashara kulipia vibali vya bidhaa wanazoingiza bila kwa urahisi.

Kaimu Meneja wa mamlaka hiyo Kanda ya Kasikazini Bwana Proches Patric amesema hatua hiyo inalenga kuondoa malalamiko ya kuwepo kwa urasimu katika vituo hivyo.

Aidha amewataka wafanyabishara kutoa ushirikiano wa kukabiliana na matatizo yaliyopo ikiwa ni pamoja na kutumia mfumo huo.

Hatua hiyo imepongezwa na baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia kituo hicho ambao wameomba  kuendelezwa kwa jitihada za kuondoa urasimu.

Kwa muda mredu sasa kumekuwepo na malalamiko ya urasimu wa kupata vibali vya kusafirisha dawa  na vifaa tiba hasa maeneo ya mipakani.