Back to top

Wabunge 4 wa CHADEMA wafikishwa Kisutu kwa amri ya Mahakama.

18 November 2019
Share


Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamuru wabunge wanne wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukamatwa leo wamefikishwa Mahakamani hapo kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Wabunge hao ambao ni washtakiwa katika kesi ya uchochezi namba 112 ya mwaka 2018 ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, John Heche mbunge wa Tarime Vijijini, Peter  Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini na Halima Mdee Mbunge wa Kawe.

Amri hiyo ilitolewa Novemba 15, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kufuatia washtakiwa hao kutofika Mahakamani hapo wakati kesi yao ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa ushahidi upande wa utetezi bila ya kuwepo taarifa zozote kutoka kwao wala wadhamini wao.

Baada ya kutoa agizo hilo hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21, 22 itakapoendelea na upande wa utetezi kuendelea na ushahidi wao.