Back to top

Wachimbaji wa madini watakiwa kutojihusisha na utoroshaji wa madini.

17 July 2019
Share


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Bwana Paul Makonda amezindua soko la kimataifa la madini mkoa wa Dar Es Salaam na kuwasihi wachimbaji na wafanyabiashara kutojihusisha na utoroshaji au utapeli wa madini.

Bwana.Makonda alianisha sababu za kufungua soko hilo katika mkoa huo ambao hauchimbwi madini na kusema kuwa licha ya mkoa wa Dar Es Salaam kuwa kitovu cha uchumi nchini pia ni lango kubwa la wageni wanaoingia na kutoka, hivyo soko hilo litaleta manufaa mbalimbali.

Kwa upande wake mwakilishi wa wafanyabiashara wa madini Bwana.Othman Tharia amewaomba wafanyabiashara wenzake waone umuhimu wa kuanzisha chama cha madini ambacho kitawatambulisha popote waendapo kama wafanyabiashara wa madini na vito kutoka mkoa wa Dar Es Salaam.

Masoko ya madini ambayo yamefunguliwa mpaka hivi sasa ni 27 na kuufanya mkoa wa Dar Es Salaam kuwa wa 28 ambapo mtaalamu kutoka wizara ya madini bw ally maganga akisema kuwa masoko hayo yataenda kutatua changamoto za wachimbaji madini na wafanyabiashara.