Back to top

Wachimbaji wadogo Mbesa waomba mtambo wa kuchenjua madini

12 June 2019
Share

Wachimbaji wadogo wa madini  katika kata ya Mbesa wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuharakisha kuwapa mtambo wa kuchenjua madini hayo ili waweze kuondokana na umaskini.

Wameyazungumza hayo wakati Tume ya madini ikitembelea eneo la mgodi wa uchimbaji wa madini aina ya Shaba katika kata ya Mbesa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kwa lengo la kuchukua sampuli kubaini kama yanapatikana madini aina hiyo pekee au kuna aina zaidi ya moja.
 
Wakiongea mara baada ya tume hiyo ya madini ikiongozwa na mwenyekiti wake, Profesa Idris Kikula, baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini katika eneo la Mbesa Tunduru wamesema kwa kipindi kirefu maisha yao ni ya umaskini mkubwa licha ya kuwa na madini ya shaba mengi lakini kikwazo kikubwa ni kukosa mtambo wa kuchenjua madini hayo.

Mwenyekiti wa tume ya madini, Profesa Idris Kikula pamoja na kamishna wa tume ya madini, Profesa. Abdulkarim Mruma wamewatoa wasiwasi wananchi pamoja na wachimbaji wadogo wa madini aina ya shaba katika eneo hilo.