Back to top

Wafugaji Kongwa walalamikia makundi ya wakulima kuvamia maeneo yao

17 November 2019
Share

Wafugaji wa vijiji vya Ngutoto,Chitego na Manyusi wilayani Kongwa mkoani Dodoma  wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi na tatu kufuatia makundi ya wakulima kutoka wilaya jirani ya Chamwino kuvamia eneo lilotengwa kisheria kwa ajili ya malisho na kufanya shughuli za kilimo hali inayohatarisha usalama wa eneo hilo

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa kujadili namna ya kutatua mgogoro huo baadhi ya wafugaji wamesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu ambapo wakulima hao wamekuwa wakivamia maeneo ya malisho na kwamba mgogoro huo umekuwa ukihatarisha hali ya usalama baina ya wakulima na wafugaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Chitego ambaye anamaliza muda wake Bw.Harold Wilson amesema mpango bora wa ardhi katika kijiji hicho ulipangwa tangu mwaka 2014 lakini kumejitokeza baadhi ya watu ambao ni wavamizi ambao wameanza kufanya shughuli za kilimo hali inayowafanya wafugaji kukosa maeneo ya malisho.

Naye mwenyekiti wa chama cha wafugaji wilaya ya Kongwa Bw. Mshando Parutu amesema sababu ya mgogoro huo kudumu kwa muda mrefu ni baadhi ya wakulima kujimilikisha maeneo makubwa katika eneo hilo ambapo amewataka wafugaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki