Back to top

Wagonjwa wafanyishwa usafi zahanati ya kijiji kabla kutibiwa Katavi.

23 June 2019
Share

Wakazi wa Kijiji cha Ilunde, Wilayani Mlele Mkoani Katavi wamewalalamikia watumishi wa zahanati ya kijiji hicho kwa kuwafanyisha kazi za usafi wanapofika kwa ajili ya kupatiwa matibabu jambo ambalo limekuwa kero kwao.

Wakazi hao wametoa malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

Akitoa majibu ya kero hiyo kwa niaba ya watumishi wa zahanati, Mtendaji wa Kata ya Ilunde, Bwana Hussein Mwita amefafanua kuwa kutokana na kuwepo kwa watumishi wachache wanalazimika kuwaomba wagonjwa kuwasaidia usafi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bwana Juma Homera amepiga marufuku suala la wagonjwa kufanyishwa kazi.