Back to top

Wakazi Dar,vaeni mavazi marefu kuzuia mbu wa Dengue.

14 May 2019
Share

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameendelea kusisitizwa juu ya uvaaji wa mavazi marefu yanayoziba sehemu ya mikono na miguu ili kuwaepusha na maambukizi ya ugonjwa wa dengue unaosababishwa na virusi vya  Dengue vinavyosambazwa na mbu aina ya Aedes ambaye hupendelea kuishi karibu na makazi ya watu na huweza kuuma binadamu mchana na usiku.

Rai hiyo imetolewa ma Mganga mkuu wa Dar es salaam Dkt. Yudas  Ndugile katika mahijiano maalum na ITV/radioone ambapo amewasihi wakati wa maeneo mbalimbali kuchukua tahadhali kubwa katika kipinid hiki cha mvua kwa kusafisha mitaro, kufukia madimbi na kusafisha maeneo yanayotuzunguka ili kujiepusha na ugonjwa huu wa dengue.

Dokta Yudas amewashauri wananchi kuwahi katika vituo vya afya mapema pale wanapohisi dalili za ugonjwa huo badala ya kunywa dawa kiholela  kwani hali hiyo inaweza kuwaletea madhara zaidi na kwamba ugonjwa wa Dengue hauna tiba yoyote ila huwa wanatibu viashiria vya dalili ambavyo mgonjwa anakuja nazo.

Mpaka sasa wagonjwa ambao wamesharipotiwa ni 1300 na wameshatibiwa na kuruhusiwa .