Back to top

Walimu nchini kupewa vishikwambi vya sensa. 

15 September 2022
Share

Serikali imesema ina mpango wa kugawa vishikwambi, vilivyotumika katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mwezi Agosti mwaka huu, kwa walimu nchini kwa lengo la kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omari Juma Kipanga, amesema hayo bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu, akijibu swali la Mbunge Subira Mwaifunga, aliyeuliza juu ya mpango mkakati wa serikali kueneza matumizi ya TEHAMA katika kufundisha ili kuwaokoa walimu na matatizo ya mgongo na shingo.

Mheshimiwa Kipanga, amesema katika mwaka 2021/22 serikali kupitia programu ya mafunzo endelevu kwa walimu kazini (MEWAKA), imewezesha mafunzo ya walimu wa shule za msingi 30400 yanayohusu matumizi ya tehama katika ufundishaji na ujifunzaji.