Back to top

Wananchi ambao maeneo yao yametwaliwa na Jeshi kulipwa fidia.

15 May 2019
Share

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussein Mwinyi amesema wizara yake inaendelea  kulipa fidia stahiki kwa wananchi ambao maeneo yao yametwaliwa na Jeshi kwa ajili ya utekelezaji wa jukumu la ulinzi wa nchi na hivyo ambao bado hawajalipwa waendeelee kuwa na  utulivu kwani zoezi la uhakiki likikamika watalipwa.
 
Mhe.Mwinyi amesema kuna maeneo ambayo tayari yamelipwa fidia na mengine mchakato wa kulipa  fidia kwa wamiliki unaendelea ingawa ni kweli kuna baadhi ya maeneo uhakiki wa fidia unaendelea kabla ya malipo kufanyka.
 
Akaongeza kuwa mpango wa serikali uliopo ni kuendelea na utaratibu wa kulipa fidia stahiki kwa wananchi kadri hali ya fedha itakavyoruhusu na kwa mujibu wa sheria ya utwaaji Ardhi kwa ajili ya matumizi ya umma.
 
Aidha Mhe.Mwinyi akaongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 wizara ilitenga shilingi bilioni 20.9 kwa ajili ya kulipa fidia maeneo yaliyotwaliwa na jeshi.
 
Mhe.Mwinyi akasema kuwa baaada ya uhakiki wa malipo ya fidia tayari kiasi cha Sh.3,005,697,801.00 kimelipwa kama fidia.