Back to top

Wananchi waomba kuharakisha ujenzi eneo la maegesho ya magari Tunduru.

22 June 2019
Share

Baadhi ya wananchi katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wameiomba halmashauri hiyo kuharakisha ujenzi wa eneo la maegesho ya magari yakiwemo malori ambayo kwa sasa yamekuwa kero kubwa kutokana na kuegeshwa maeneo mbalimbali ya barabarani na makazi ya watu hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa wananchi.
 
Baadhi ya wananchi hao katika mji huu wa Tunduru mkoani Ruvuma, wametoa ombi hilo kufuatia kukithiri kwa magari mbalimbali yakiwemo malori kuegeshwa kando kando mwa barabara na makazi ya watu hali ambayo wamedai inaweza kuhatarisha usalama wa maisha ya wananchi.
 
Hata hivyo akizungumza na ITV,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru,Bw.Gaspar Balyomi amesema tayari ujenzi wa eneo la kwa ajili ya maegesho ya magari hayo unaendelea na kwamba magari yote yakiwemo ya mizigo yatapaswa kushushia mizigo katika eneo hilo na si vinginevyo.