Back to top

Wasichana waozeshwa kwa marehemu ili kukuza ukoo mkoani Mara.

13 November 2019
Share

Wasichana mkoa wa Mara wanaozeshwa kwa wanaume waliokufa wakiwa hawajaoa ili kukuza ukoo wa marehemu hao ikiwa ni sehemu ya mila na desturi za makabila ya mkoa huo hususani kabila la Wakurya.

Mkoa wa Mara, usioisha vituko na vioja, hiki nacho ni kioja kingine hususani kwa kabila la Wakurya ambapo wasichana wadogo walio na uwezo wa kuzaa huozeshwa kwa wanaume waliokufa kabla hawajoa na kuitwa wake wa marehemu ikiwa ni sehemu ya mila inayolenga kukuza ukoo wa kijana anayekufa bila kuoa wala kuzaa mtoto.

Hadija Isaro ni miongoni mwa kundi la wasichana Wakikurya aliyeozeshwa kwa mtu aliyekufa Chacha Ntakamazi ambaye aliuawa kwa kuchomwa kisu tumboni mwaka 2013 ambapo mwaka 2014 Hadija akiwa na umri wa miaka 15 aliolewa na marehemu huyo pasipo kujua kwa mahari ya Ng'ombe 11 huku akihadaiwa na wazazi kuwa ameolewa na kaka wa marehemu na kudai mila hiyo ni mbaya.

Bwire Mwinuko na Samson Riyoba ni wazee wa mila katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mkani hapa wanasema kwa mujibu wa mila na desturi za kabila hilo kijana wakiume anapofariki bila kuoa na akaacha mali ni lazima ukoo utafute msichana atakayekuja kuolewa kwenye mji wa kijana huyo na kujulikana kama mke wa marehemu ambapo msichana anaweza kutafuta mwanaume nje akazaa watoto wakaitwa watoto wa marehemu au akatafutiwa mume ndani ya ukoo hasa kaka wa marehemu ambaye ameoa na kumuolea marehemu.

ITV ilizungumza na mtaalam wa saikolojia na kiongozi wa dini ili kufahamu madhara ya mila hii ambapo wamesema inawadhalilisha wasichana na inamadhara kwa watoto na wanawake na kwamba ni chukizo mbele za mungu.