Back to top

Watanzania watumie fursa ya upungufu wa nafaka kujiwekea akiba.

14 September 2019
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watumie fursa ya upungufu wa nafaka katika nchi za Kusini mwa Afrika kwa kuzalisha zaidi mazao hayo ikiwa ni pamoja na kujiwekea akiba zaidi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa akihirisha Mkutano wa 16 wa Bunge jijini Dodoma hadi Novemba 5, mwaka huu na kusemma hali ya usalama wa chakula katika ukanda wa Jumuiya ya Maende leo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Amesema upatikanaji wa chakula kwa nchi hizo imetetereka kutokana na athari mbalimbali ikiwemo ukame kwa upande wa magharibi wa ukanda, mvua zilizokithiri, mafuriko na vimbunga vya IDAI na Kenneth pamoja na wadudu waharibifu wa mazao na magonjwa.

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa amesema kuwa Agosti 29-30, mwaka huu, Wizara ya Kilimo iliratibu mkutano na wadau mbalimbali wenye kujihusisha na uzalishaji na biashara ya nafaka ili kujadili fursa zilizopo katika mazao ya nafaka, changamoto wanazokabiliana nazo na kutafuta utatuzi wake.

Pia ameitaka wizara hiyo iendelee kuhamasisha uzalishaji wa mazao hayo kwa wingi ili nchi iweze kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada kwa wananchi hapa nchini.