Back to top

Watu 40 wauawa, 20 wajeruhiwa katika shambulio la risasi New Zealand.

15 March 2019
Share

Watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya kufuatia shambulio la risasi lililotokea katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch nchini New Zealand.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Jacinda Ardern amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo ambapo hadi sasa wanaume watatu na mwanamke mmoja wanashikiliwa na polisi na msako bado unaendelea kuwatafuta wengine waliohusika na tukio hilo.

Misikiti yote katika mji huo imeagizwa kufungwa hadi hapo watakapopewa utaratibu mwingine.