Back to top

Watumishi 32 wa wilaya ya Sikonge wafukuzwa kazi

29 May 2020
Share

Baraza  la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora limewafukuza  kazi watumishi thelathini na mbili ambapo kati yao ishirini na tisa wakiwa ni waalimu pamoja na watendaji  watatu wa kata na vijiji baada  ya kuhusika na tuhuma mbalimbali ikiwemo upotevu wa fedha zaidi ya  shilingi milioni 50 za  mapato ya ndani ya  halmashauri hiyo.

Akizungumza mara baada ya maamuzi hayo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge  Peter Nzalalila amesema baraza limejiridhisha kuwa miongoni mwa watumishi hao wamekuwa na vyeti vya kughushi huku watendaji wa kata na vijiji wakikwama  kwa kipindi cha miaka miwili kurejesha makusanyo ya mapato ya ndani ambayo wamekuwa wakikusanya

Baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wamelipongeza baraza la madiwani kuchukua hatua hiyo ambapo pia wakatumia fursa hiyo kuomba serikali kuanza kutoa huduma za awali katika hospitali ya wilaya iliyokamilika na kushindwa kuanza kutoa huduma