Back to top

Wawili wajeruhiwa kwa taharuki ya moto katika bank ya NMB.

16 November 2019
Share

Moto uliozuka katika benki ya NMB tawi la Mpanda mkoani Katavi umezua taharuki kubwa kwa wateja waliokuwa wakihudumiwa ndani ya benki hiyo na kusababisha majeruhi wawili ambao wamepelekwa kupata matibabu katika hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Katavi.


Kaimu Meneja wa benki ya NMB tawi la Mpanda Highgrace Mwanjuguja amesema tukio hilo lilikuwa ni jaribio la ajali ya moto ili kutoa elimu ya uokoaji kwa wananchi.


Kwa upande wake Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokozi mkoa wa Katavi Gabriel kutiku ametoa wito kwa wananchi kujifunza namna ya kujiokoa kutoka katika majanga mbalimbali ikiwemo moto.