Back to top

Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi saba.

15 September 2019
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika halmashauri mbili za wilaya ya Kilombero na  kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya sh. bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.
 
Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara  Fransis Ndulane anayedaiwa  sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.
 
Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha oleo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.
  
Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara  makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7  ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9   na kwamba kiasi cha  shilingi milioni 727  hazijulikani zilipoenda. 
 
Amesema katika mitambo kumi  ya ukusanyaji wa mapato iliokaguliwa imeonyesha kiasi cha shilingi milioni 348 zilizokusanywa hazikupelekwa bank na hivyo kuishia mikononi mwa watu.
 
Waziri Mkuu amesema katika uchunguzi huo ilibainika kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti mbalimbali za watumishi wa halamshauri hizo  kutoka kwa mtendaji wa Kata ya Viwanja 60 katika Mji wa Ifakara aitwaye Gregory Midas.
 
Watumishi   hao ni  Reina Mrema ambaye anadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 298, Haile Njitango milioni 73 , Linus Mdembo kiasi cha shilingi milioni 2 kwa kushirikiana na mtendaji huyo wa Kata.
 
Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika halmashauri ya Mji wa Ifakara, John Mvanga ambaye ndiye alibaini kuwepo na ubadhilifu wa fedha hizo na badae kusimamishwa kazi, arejeshwe kazini mara moja na asibugudhiwe.