Back to top

WAZIRI UJENZI APEWA ZAWADI KWA KUTIMIZA AHADI YA SAA 72 KILWA.

29 May 2024
Share

Waziri wa Ujenzi Mh. Innocent Bashungwa akikabidhiwa zawadi ya jogoo,  kwa juhudi kubwa za urejeshaji wa mawasiliano ya Barabara katika eneo la Tingi – Kipatimo, na Barabara Kuu inayounganisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara.

Zawadi hiyo imetolewa  na Mzee Kimbwembwe kutoka Kijiji cha Somanga, ikiwa ni saa chache kabla ya Bashungwa kuwasilisha bajeti yake bungeni kwa mwaka 2024/25.

 Julai 30, 2020 Mzee Kimbwembwe alimkabidhi zawadi ya jogoo Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt John Pombe Magufuli alipopita katika eneo hilo ambapo alimshukuru kwa kuwapelekea kituo cha afya.

“Na wewe Bashungwa (Waziri wa Ujenzi) kwa kauli moja sisi wananchi wa Kilwa tumekuletea zawadi hii kutokana na kazi kubwa uliyoifanya kwa kurudisha mawasiliano ndani ya saa 72 kama ulivyoahidi,” amesema.

Mzee huyo amesema kilichowafurahisha wananchi wa huko ni kitendo cha Waziri kukaa huko kwa siku tano akishughulika na urudishaji miundombinu iliyokatika kwa sababu ya mvua kubwa jambo linaloonyesha kujali.