Back to top

Zana haramu 5,525 za uvuvi zateketezwa kwa moto Busega.

22 June 2019
Share

Zana haramu za uvuvi zipatazo 5525 pamojana na kamba za kokoro zenye urefu wa mita 163,950zilizokamatwa na kikosi cha doria kanda ya Simiyu na Magu zikitumika kuvua kinyume cha sheriaya uvuvi  namba 22, 2003 katika mialo ya wilaya za Busega mkoani Simiyu na Bunda mkoani Mara zimeteketezwa kwa moto.

Akizungumzia zoezi hilo  afisa mfawidhi wa uvuvi kanda ya Simiyu na Magu, Samson Mboje anasema pamoja na manufaa ya kiuchumi kwa wananchi wanaolizunguka ziwa Victoria na taifa kwa taifa kwa ujumla rasilimali ya uvuvi inatishwa na uvuvi haramu kwa kutumia zana zilizopigwa marufuku.

Mkuu wa wilaya ya Busega Tano Mwera ambaye ndiye aliongoza zoezi la kuteketeza zana hizo amewataka wavuvi wote wilayani  Busega waache kulalamika kila jambo kwamba wanaonewa badala yake watii sheria bila shuruti kwa kuacha uvuvi haramu.

Kaimu hakimu wa mkoa wa Simiyu Mary mrio amesema jukumu la kulinda ziwa Victoria ni la kila mwananchi ambapo amewataka wavuvi kuvua kwa kufuata sheria na kwamba mahakama haitamuonea huruma yeyote atakayekamatwa na zana haramu