Back to top

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI, UPANUZI MSIKITI MKUU WA IJUMAA TANGA

26 February 2025
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Februari 26, 2025, ameongoza hafla ya kihistoria ya kuweka jiwe la msingi kwaajili upanuzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa jijini Tanga, tukio ambalo lilihudhuriwa na viongozi wa dini wakiongozwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Abubakary Zubeiry bin Ally, viongozi wa serikali, waumini na wananchi wengi kutoka sehemu mbalimbali.

Rais Samia ametoa fursa hiyo kutoashukrani maalum kwa uongozi wa Lake Group kwa kujitolea kwa kuwekeza nguvu zao katika ujenzi wa msikiti huo, ambao utakuwa na faida kubwa kwa jamii ya Kiislamu na kwa maendeleo ya Tanga kwa ujumla.

Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa mshikamano kati ya serikali na jamii katika kuleta maendeleo, akisema kuwa dua za viongozi wa dini na juhudi za serikali zitatufanya tuendelee kuwa taifa lenye umoja na mafanikio. 

Ametumia mfano wa marehemu Sharif Haidary bin Ahmed, ambaye alitoa wakfu wa ardhi yake kwa manufaa ya vizazi vijavyo, akisisitiza kwamba wengi wetu tunapaswa kutazama maisha kwa upana zaidi na kuwazia vizazi vya kesho.

Aidha, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa taasisi za dini katika kukuza maadili na kuhamasisha kupambana na changamoto kama vile matumizi ya dawa za kulevya, na kuahidi kusaidia juhudi za kuchangia ujenzi wa uzio wa makaburi ya Msambweni.

Rais Samia amebainisha kuwa, mradi huo unatarajiwa kugharimu bilioni sita za Kitanzania, akieleza kwamba huo ni mradi wa kipekee utakaoongeza haiba ya mji wa Tanga na kuimarisha sekta ya elimu na dini.