Back to top

Guardiola aitaja Liverpool kuwa chanzo cha ushindi wake.

14 May 2019
Share

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ambao ni mabingwa wa ligi kuu Uingereza msimu huu wa 2018/19 amewashukuru wapinzani wake klabu ya Liverpool kwa namna walivyokuwa wakimpa presha ya kupambana kwenye kila mechi.

Man City msimu huu wametwaa kombe wakiwa na tofauti ya alama moja na Liverpool.

Wakati huohuo, uongozi wa timu ya Brighton & Albion umemtimua kocha wake Chris Hughton siku moja baada ya kufungwa na Manchester City licha ya kuinusuru timu hiyo kushuka daraja msimu 

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Tony Bloom kwenye taarifa yake ameeleza, Hughton amefanya kazi nzuri kwa miaka minne iliyopita hata hivyo wamelazimika kuachana nae.