Back to top

Kigwangala aongoza mbio za Serengeti Marathon.

16 November 2019
Share

Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dr Hamisi Kigwangala leo ameongoza wanariadha zaidi ya 700 kutoka mataifa mbalimbali katika mashindano  ya riadha ya Serengeti Marathon yaliyofanyika katika hifadhi ya Serengeti geti la Ndabaka ambapo amesema mbio hizo kwa mwaka huu zimefana sana tofauti na mwaka jana na kuahidi kuziboresha zaidi mwakani.

Mkurugenzi wa Serengeti Marathon ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo Timoth Mdinka amesema  mashindano hayo yanafungua fursa za utalii katika ukanda wa Magharibi mwa Serengeti.