Back to top

'The Special One' ateuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Tottenham

20 November 2019
Share

Jose Mourinho 'The Special One' ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya  Tottenham kwa mkataba utakaomuwezesha kudumu katika klabu hiyo hadi mwaka 2023.

Mourinho alizifundisha timu kama Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid na Manchester United huku akishinda taji la  UEFA Champions League mara mbili, Europa League mara mbili na makombe ya ligi mara nane.

Mara ya mwisho aliondoka katika klabu ya Manchester United baada ya kutimuliwa na kuwa Mchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha Sky Sports.


Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesema kumchukua Jose Mourinho wamepata moja kati ya mameneja wenye mafanikio kwenye soka,anauwezo mkubwa na uzoefu na anaweza kuwashawishi wachezaji katika mbinu.

"Ameshinda mataji makubwa karibu katika kila timu aliyoifundisha, kwaiyo tunaamini kuwa ataleta nguvu ya timu na hamasa kwenye vyumba vya kubafilishia nguo kwa wachezaji".


Akizungumza baada ya kupewa kazi hiyo Mourinho amesema kuwa anafurahi sana kujiunga na klabu hiyo yenye urithi mzuri na mkubwa na mashabiki wenye moyo wa dhati .

Tottenham watacheza dhidi ya West Ham Jumamosi hii na Mourinho anatarajiwa pia kukutana na timu yake aliyoifundisha ya Manchester United ifikapo tarehe 4 mwezi Desemba.