Back to top

ATAPELIWA ZAIDI YA MIL. 100 NA ELON MUSK BANDIA

03 May 2024
Share


Mwanamke mmoja nchini Korea Kusini, aliyejulikana kwa jina la Jeong Ji-sun, ametapeliwa zaidi ya Dola za kimarekani 50,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 100 za Kitanzania, na tapeli ambaye alijitambulisha kuwa ni Bilionea Elon Musk, kupitia mtandao wa Instagram.
.
Ji-sun amesema, licha ya yeye kuwa shabiki mkubwa wa Bilionea huyo, lakini kwake ilikuwa kama ndoto, baada ya kuona Elon Musk, amemfuatilia kwenye ukurasa wake wa Instagram, na kwamba baada ya kusoma wasifu wake, mwanzo alipata mashaka, lakini mashaka yake yalitoweka baada ya tapeli huyo kumtumia picha akiwa kazini na kuna wakati walikuwa wakizungumza kupitia video (video call).
.
Amesema Baadae tapeli huyo alimshawishi kuhamishia kiasi hicho cha fedha kwenye akaunti ambayo alidai kuwa ni ya mfanyakazi wake aliyepo Korea Kusini na alimuahidi kuwa atamtajirisha kwa kuwekeza pesa zake kwake ambapo alimwambia kuwa yeye hufurahia sana akiona mashabiki wake wanatajirika.  
.
Lakini baadae ilikuja kugundulika kuwa Ji-sun, aliingia kwenye mtego wa utapeli kwa njia ya Artficial Intelligence (AI), hali iliyomsababishia hasara kubwa ya kifedha na ameshindwa kupata msaada kutokana na sheria za Korea Kusini kukosa vifungu vinavyoweza kuzuia uhalifu kama huo. #via #NDTVWorld