
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi ( CCM),CPA Amos Makalla amewaonya baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali ya chama wanaowahakikishia ushindi watia nia wa ubunge na udiwani, akiwataka kuacha mtindo huo, kwa kuwa wao si wenye uamuzi wa mwisho.
CPA Makalla amewafananisha viongozi hao ni sawa la wale wanaofanya 'betting' (mchezo wa bahati nasibu), akisema wakati wowote mkeka utachanika na watashindwa kuwaambia wagombea wao mambo yakiwa kinyume.
Ameeleza hayo wakati akizungumza na viongozi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kibaha Mjini katika uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa llani ya CCM jimbo hilo mkoani Pwani.
"Safari tumekuja na uratibu utakaohakikisha wagombea watakaoteuliwa wanakubalika, ukiendelea kuwaahidi kwamba nafasi ya ubunge una uhakika nayo, ukiwa wilayani au mkoani basi ujumbe kuna kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM Taifa," amesema Makalla.
Amewataka viongozi wa CCM kupunguza ahadi na kuwabeba wagombea, badala yake watenda haki na usawa kwenye uwanja wa mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho tawala nchini