Back to top

2025 TANZANIA MWENYEJI KONGAMANO LA VYAKULA VYA ASILI

27 July 2024
Share

Tanzania inatarajiwa kuwa Mwenyeji, wa Kongamano la Pili la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Kanda ya Afrika kuhusu utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Afrika kwa mwaka 2025.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism), Zurab Pololikashvili katika ufunguzi wa Kongamano la kwanza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, Kanda ya Afrika kuhusu Utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Africa (Gastronomy) linaloendelea jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe .

Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, amesema kufanyika kwa kongamano hilo  nchini Tanzania,  kutakuwa na manufaa makubwa katika kukuza mnyororo mzima wa thamani katika utalii, ikiwemo Utalii wa vyakula hasa kugusa wadau wengi wakiwemo wakulima wafugaji, wavuvi,wazalishaji wa nafaka,wachakataji wa mafuta .