Back to top

ACHAPWA VIBOKO 12 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI MWENZAKE

27 September 2024
Share

Hija Hamis Msumi (16) Mwanafunzi ya Kidato cha Tatu, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti, mkoa wa kipolisi Rufiji, amehukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko 12, kwenye makalio mbele ya mahakama kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la Nne mwenye umri wa miaka 12.

Mahakama imemuamuru mshitakiwa huyo kumlipa muhanga fidia ya Shilingi laki 5, kwa madhara ambayo amemsababishia mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mahakama imesema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya mwezi Agosti na Novemba, 2023, huko Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti.