Back to top

Afisa Madini mkoa wa Arusha atumbuliwa, Biteko anena

14 November 2019
Share

Waziri wa madini Mhe.Dotto Biteko amemsimamisha kazi  afisa madini  mfawidhi mkoa wa Arusha Robert Erick  kwa uzembe wa kushindwa kusimamia wafanyabiashara wa  madini kuingia kwenye soko la madini na kusababisha wafanyabiashara kuendelea kutorosha madini huku akiagiza wafanyabiashara wote wawe wameamia kwenye soko hilo hadi ifikapo jumatatu ya wiki ijayo

Mhe.Dotto Biteko ametoa maamuzi hayo alipofanya ziara kwenye soko la madini  la mkoa wa Arusha na kugundua mapungufu hayo

Awali katibu mkuu wizara ya madini Prof.Simon Msanjila alieleza masikitiko yake  kuhusu hali hiyo  huku wafanyabiashara wa madini wakawakilisha changamoto zinazowakabili.