Back to top

AGIZO LA SAMIA LATEKELEZWA, RASMI FEISAL NI MALI YA AZAM FC

08 June 2023
Share

Klabu ya Yanga SC imetangaza kumuuza mchezaji wake Feisal Salum kwa timu ya Azam FC, baada ya pande zote kufikia makubaliano kwa kuzingatia matakwa ya kimkataba kati ya klabu na mchezaji.
.
Hata hivyo timu hiyo imesema bei aliyouzwa mchezaji huyo haitwekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
.
Maamuzi hayo yamefiuata ikiwa ni siku chache tu baada ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kuitaka timu ya Yanga SC kumalizana na Feisal.