Back to top

Ajali ya ndege yaua Rubani na Abiria wake Serengeti mkoani Mara.

23 September 2019
Share

Watu wawili wamefariki dunia  baaada ya ndege ya kampuni ya Auric Air kuanguka katika uwanja mdogo wa ndege Seronera , katika hifadhi ya taifa Serengeti Mkoani Mara.

Kwa mujibu wa taarifa za awali Ndege iyo imedondoka wakati inaruka baada ya hitilafu katika uwanja huo.

Meneja mawasiliano wa shirika la hifadhi za Taifa TANAPA Pasko Shelutete amethibitisaha kutokeakwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wawili RUBANI NA ABIRIA waliokuwa wakisafiri kutoka Serengeti mara kwenda Arusha.

Shelutete amesema Taarifa rasmi ya chanzo cha ajali hiyo itatolewa Mamlaka ya usalama wa anga na kampuni husika ya ndege baada ya kujua chanzo uchunguzi utakapokamilika.