Back to top

AL AHLY YACHAPWA 4-3 NA ZAMALEK FAINALI CAF SUPER CUP

28 September 2024
Share

Wafalme wa soka la Afrika Al Ahly, wamefurushwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Zamelek, katika mchezo wa Fainali ya CAF Super Cup, uliopigwa usiku wa Septemba 27, 2024 kwenye Uwanja wa Kingdom, uliopo katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Awali, Al Ahly walipata bao la kuongoza dakika ya 44 ya mchezo kabla Nasr Mansi wa Zamalek, kuja kusawazisha dakika ya 77 ya mchezo na dakika 90 kumalizika kwa sare hiyo ya 1-1 hivyo kuingia kwenye mikwaju ya penalti.

Mchezo huo uliwakutanisha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika.

Al Ahly walitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuishinda Esperance Sportive de Tunis, katika fainali iliyofanyika Mei 25, 2024.

Zamalek walitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho baada ya kuishinda RS Berkane katika fainali ya Mei 19, 2024.