
Mwanahabari wa Italia Giulia Cortese ameamuliwa kumlipa Waziri Mkuu Giorgia Meloni fidia ya Euro 5,000 kutokana na machapisho ya mitandao ya kijamii yanayodhihaki kimo cha waziri mkuu huyo.
Jaji aliamua kwamba jumbe mbili za Giulia katika mtandao wa kijamii zilikuwa za kumchafulia jina Waziri mkuu na zilidhamiria ‘kumuaibisha’ kwa sababu ya mwili wake.
Ilifuatia mazungumzo ambayo Bi Cortese alimtaja Bi Meloni kama "mwanamke mdogo, na siwezi hata kukuona."
Akijibu uamuzi huo, Bi Cortese alisema serikali ya Italia ina "tatizo kubwa la uhuru wa kujieleza na upinzani wa waandishi wa habari".
Wawili hao waligombana kwa mara ya kwanza mnamo Oktoba 2021, wakati chama cha Bibi Meloni cha Mrengo wa kulia cha Brothers of Italy kilikuwa bado katika upinzani, baada ya Bi Cortese kuchapisha picha ya dhihaka ya Bi Meloni kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter.
Baadaye tena katika chapisho hilo mwandishi huo aliandika tena "Hunitishi, Giorgia Meloni, kabla ya yote, una urefu wa 1.2m [3ft 9in] tu, Siwezi hata kukuona."
Urefu wa Bi Meloni unaripotiwa katika vyombo vya habari vya Italia kuwa 1.63m (5ft 3in).
