Back to top

Aliyewakeketa wasichana zaidi ya 200 anaswa na nyembe zaidi ya 50.

19 November 2019
Share

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Tarime mkoani Mara inamshikilia mkazi wa kijiji cha Nyamwaga January Matiko, baada ya kumkuta na visu vinane na nyembe zaidi ya hamsini vitu ambavyo amekiri kuwa amevitumia kwa kuwakeketa zaidi ya wasichana mia mbili.

Hatua hiyo imefuatia msako wa kuwatafuta wahalifu wanaofanya vurugu na kuua watu kwa madai ya kujiandaa kuelekea kwenye shughuli za ukeketaji.

Baadhi ya wazazi wameiomba  serikali kuendelee kuvitokomeza vitendo hivyo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Henry Mwaibambe amesema jeshi hilo limeanza kuwakamata vijana wanaofanya vurugu kwa madai kuwa ni maandalizi ya kuelekea jandoni.