Back to top

Bajeti kuu ya Trilioni 33 nukta moja kuwasilishwa leo.

13 June 2019
Share

Leo ni Bajeti, Siku ambayo Serikali inatarajia kuwasilisha Bungeni bajeti kuu ya Shilingi Trilioni 33 nukta moja, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 wakati baadhi ya wabunge wakitaka sera za fedha zijikite katika uzalishaji wa ajira na bidhaa ili kuongeza mapato yanayotokana na kodi.

Baadhi ya Wabunge wameitaka serikali kutekeleza kauli ya Rais ya kupunguza utitiri wa kodi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji ili kufikia utekelezaji wa malengo ya miradi ya maendeleo.