
Mahakama ya Wilaya ya Iramba, imemuhukumu kifungo cha maisha Jela, Barnaba Yohana Isaya (20), mkazi wa kijiji cha Nselembwe ,kata ya Sherui, Wilaya ya Iramba Mkoani Singida kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume miaka minne (4) Mkazi wa kijiji hicho.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama hiyo, Mhe. Simon Kayinga, ameeleza kuwa baada ya Mahakama kujiridhisha pasi na shaka na maelezo ya mashahidi, mshitakiwa ametiwa hatiani na atatumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa hilo la ukatili.
Mtuhumiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi Februari 5, 2024 katika kijiji cha Nselembwe, ambapo alifikishwa Mahakamani Februari 12, 2025 kujibu tuhuma zinazomkabili, ambapo Mhe. Kayinga amesema adhabu hiyo ikawe fundisho kwa watu wenye tabia za ukatili kama huo.