Siku mbili baada ya jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kupiga marufuku maandamano ya baraza la wanawake wa CHADEMA mkoa wa Geita kwa madai kuwa hayajafuata utaratibu, Baraza hilo limeliomba jeshi hilo kulinda maandamano hayo kwa kuwa ni ya amani na hayana vurugu na yanalenga kuonana na kufikisha ujumbe kwa Spika wa Bunge Mhe.Jobu Ndugai.
.
Mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Geita Bi.Helena Thobiasi amesema maandamano hayo ni ya amani na yanahusisha wanachama kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.