Back to top

BENKI YA CRDB YATOA TUZO KWA WALIMU - RUNGWE.

04 July 2024
Share

Katika kuhakikisha kiwango cha elimu bora kinakuwa nakuleta tija kwa wanafunzi,Benki ya CRDB, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imetoa tuzo za pongezi kwa walimu 8 kutoka shule mbalimbali wilayani Rungwe, mkoani Mbeya, ambao masomo wanayofundisha katika shule zao yamefanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kwa mwaka wa masomo uliopita.
 
Afisa uhusiano wa benki hiyo katika kanda hiyo Bi. Paschalina Diu, amesema benki ya CRDB, inatambua mchango mkubwa wa walimu katika kuinua sekta ya elimu kwa kutumia ubunifu mbalimbali ili kuongeza uelewa kwa wanafunzi hivyo wameamua kutoa tuzo hizo ili kuongeza motisha kwa walimu hao.
 
Katika tukio hilo lililoambatana na maadhimisho ya siku ya elimu, katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, ambapo pia tuzo zingine zimetolewa kwa walimu, wanafunzi na wadau wa elimu, Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Jaffar Haniu, mbali na kuwataka walimu kuongeza juhudi ili kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda amepongeza utolewaji wa tuzo hizo.