Back to top

BENKI YA TAIFA YA USHIRIKA KUANZISHWA HIVI KARIBUNI.

04 July 2024
Share

Wanaushirika wametakiwa kuendelea kuchangia Mtaji wa Uanzishaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika kwa kununua hisa za Benki hiyo.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Omar, katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani  yanayoendelea katika viwanja vya Ipuli, Mjini Tabora.

Dk. Omar amesema ni muhimu kwa wanaushirika kuwa na Benki yao, Hali itakayowasaidia kuwa sehemu ya maamuzi ya Benki hiyo, pamoja na kusaidia uchumi wetu kufikia kiwango cha uchumi wa juu wa kati ifikapo 2050 kupitia Kilimo na Ushirika.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Meneja Mkuu wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro, Godfrey Ng'urah, amesema tayari hatua muhimu za uanzishaji wa Benki hiyo zimekamilika na kwamba yamebaki masuala machache ambayo yanatarajia kukamilika hivi karibuni. 

Benki hiyo ya Taifa ya Ushirika itaundwa na muunganiko wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro pamoja na Benki ya Ushirika ya Tandahimba.